welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday, 12 October 2014

MSANII JACKIE WOLPER ATEMA CHECHE! Wr

                       Mtoto mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper.

MTOTO mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper, amemtolea uvimu pedeshee maarufu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu na kumwambia aache kumfuatafuata.Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkongo huyo ambaye anajitapa kuwa ameshatembea na baadhi ya mastaa Bongo akiwemo Wolper, alikaririwa katika gazeti hilihili akidai ametembea na Wolper kisha kumwaga na sasa anammendea mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote. 
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema anamshangaa mwanaume huyo amekuwa akimfuatafuata na kumzungumzia katika vyombo vya habari wakati hana hadhi ya kuwa na mtu kama yeye.
Jacqueline Massawe Wolper.
“Kwangu mimi huyo mwanaume siyo hadhi yangu, ni mshamba, limbukeni asiyeweza kuniweka mjini…kifupi nimwambie akome kunizungumzia mimi siyo taipu yake, atafute wa saizi yake,” alisema Wolper na kuongeza: 
“Nilikutana naye Nairobi aliposema ana shida ya kikazi ndiyo akaanza kuleta mambo ya kunitongoza, nilipomfuatilia nikaona si mtu mzuri, hazimo kidogo. Huwezi kuwa mwanaume ambaye unaropokaropoka hovyo, mimi nina mtu wangu namuheshimu, akome kunizungumzia.”

No comments: