welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday, 9 October 2014

MASTAA KIBAO WAKIJIACHIA KWENYE BIRTHDAY YA ROSE NDAUKA WA BONGO MUVI!


Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni usiku wa furaha kwa staa wa Filamu Bongo, Rose Ndauka, kwani aliweza kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na baadhi ya mastaa wenzake waliyofurika ndani ya Hoteli ya Collossium iliyopo maeneo ya Kamata Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rose Ndauka (kushoto), akimlisha kipande cha keki rafiki yake mpendwa Jack Pentzel, muda mfupi baada ya zoezi la kulishana keki kuanza kwenye sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Collosseum Hoteli Kamata Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rose akimlisha keki mwigizaji mwenzake Mayasa Mrisho 'Maya'.
Mwigizaji Jimmy Mafuvu akilishwa keki hiyo na Rose Ndauka.
Maya akifungua shampeni kama ishara ya upendo kwa Rose Ndauka ambaye alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa.
Rose Ndauka akimnywesha shampeni Jack Pentzel.
Rose akiselebuka na baadhi ya marafiki zake.
Rose (kulia), akivishwa pete ya dhahabu na dada ake ikiwa kama moja ya zawadi yake katika kusrekea siku ya kuzaliwa kwake.
Jack Pentzel akimmiminia noti Rose Ndauka kama moja ya zawadi yake.
Rose Ndauka akionyesha pete aliyovikwa mkono wa kulia kwake kama moja ya zawadi iliyotoka kwa dada yake.
Mtangazaji wa Times FM, Hadija Sahib 'Dida', akiselebuka na rafiki yake kwenye pati hiyo.
Rose Ndauka akiwa kwenye pozi la pamoja na baadhi ya ndugu na marafiki zake.
Dida akiwa katika pozi na dada yake Rose.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakicheza moja ya muziki uliyokuwa ukipigwa kwenye sherehe hiyo na Rose Ndauka.
Rose Ndauka na baadhi ya waarikwa wakigonga chairs mara baada ya kufungua shampeni iliyokuwa imeandaliwa kwenye sherehe hiyo.

No comments: