welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday, 16 October 2014

MAMENEJA WA T.I KUJA KUTOA SEMINA YA MUZIKI DAR


T.I akiwa na manager wake Jason Geter 
Ikiwa ni siku chache tu zimebakia ili shangwe za Serengeti Fiesta zitawale katika maskio ya wakazi wa Dar es Salaam, October 18, Meneja wa T.I., Jason Geter pamoja na meneja wa Wizkid na Waje, Cecil Hammond, wanatarajia kutoa semina kwa wadau wa muziki itakayofanyika ijumaa hii. Akizungumza Mtandao huu leo 
mwenyekiti wa tamasha la Serengeti Fiesta 2014, Sebastian Maganga, amesema meneja wa T.I. na yule wa Waje wanatarajia kuingia Jumatano, October 15 ili kujiandaa na shughuli mbalimbali ikiwemo semina pamoja na kufungua duka litakalouza kazi za T.I. 
“Mpaka sasa ratiba inaenda vizuri, meneja wa T.I ‘Jason Geter’ na meneja wa Waje na Patoraking, wanatajia kuingia usiku wa Jumatano, kwa sababu kama meneja wa T.I. anakuja mapema ili kuangalia mazingira na atakuwa na semina na wadau wa muziki kuzungumzia jinsi muziki au msanii unavyoweza kutumia jina lako kibiashara. Pia atafungua duka ambalo litakuwa linauza productiob za T.I. Pia meneja wa Waje ‘Cecil Hammond’ atakuwepo kwenye semina hiyo,” alisema Sebastian Maganga.
Cecil Hammond
Pia Sebastian alisema wasanii wa kimataifa wanaotarajia kupagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta ni T.I, kutoka Marekani, Waje na Patoraking kutoka Nigeria pamoja na Victoria Kimani kutoka Kenya. Pia amedai kuna msaani mmoja mkubwa kutoka Nigeria ambaye bado wapo kwenye mazungumzo na jibu ramsi litapatikana kesho mchana.
“Katika wasanii wa kimataifa T.I. ataingia Dar Ijumaa usiku,” amesema.
Wasanii wa Bongo wanaotarajia kupanda jukwaa moja na wakali hao kutoka nje ni, Diamond, Alikiba, Ommy Dimpoz, Mr Blue, Stamina, Nay wa Mitego, Vanessa Mdee, Mwana FA, Weusi,Young Killer Msodoki, Linah Sanga, Recho, Barakah Da Prince, Mo Music, pamoja na Super Nyota G.Luck, K. Style pamoja na Edu Boy.
CDT:BONGO 5

No comments: