welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday 16 October 2014

FASTJET SASA NI KIMEO AU?

Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Fast Jet.
SHIRIKA la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na wateja wake mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi Jumatano lina habari kamili.Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wateja hao wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa shirika hilo linatoa huduma ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii, kwani tiketi zinazouzwa kwa bei hizo ndogo, daima huelezwa kuwa zimekwisha.
“Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini Mwanza.
Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet, lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
“Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.
Abiria wakishuka kutoka kwenye ndege ya Fast Jet.Alisema shirika hilo la ndege lina utaratibu unaomuumiza mteja hasa pale anapoahirisha safari au kuchelewa ndege, tofauti na mashirika mengine kama Precision Air na Air Tanzania.
“Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.
“Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.
“Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende nikachukue simu yangu.
Marubani wa ndege ya Fast Jet wakiwa mzigoni.“Wakaniambia wao hawana mamlaka ya kuingia ndani ya ndege ile, badala yake wakanisaidia

No comments: