welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Friday 17 October 2014

MAKAVU LIVE: JOHARI, CHUCHU HUU KAMA SIYO USHAMBA NI NINI?

NINAMFAHAMU Blandina Changula maarufu kama Johari, tokea akiwa underground wa maigizo katika kikundi cha Kaole, kabla hajapata jina linalomfanya kuwa mmoja wa wakongwe katika filamu Tanzania.
Wakati ule akichipukia, alikuwa mmoja kati ya chipukizi waliokuwa wanaonyesha wazi kwamba watakuja kuwa waigizaji wazuri. Anapatia sehemu nyingi katika sanaa, lakini utampenda zaidi Johari akiigiza sehemu inayohitaji majonzi, au mtu anayetaka kuhurumiwa. 

Johari anaweza kutoa machozi wakati wowote akitaka. Anaweza kucheka kwa sauti na furaha dakika hii, lakini inayofuata akatoa machozi mengi hadi unashangaa. Napata wasiwasi ninapomuona akitoa machozi katika misiba, hujiuliza kama analia kweli kwa uchungu au ni mbwembwe tu za maigizo ili watu wajue ana uchungu! Kama nilivyosema mwanzo, Johari ni mmoja kati ya waigizaji wasichana ninaowafahamu zaidi katika fani, pengine kuliko masistaduu wengi waliopata majina makubwa katika miaka ya hivi karibuni. Anajua kufanya kazi kwa kweli na ni lazima hawa waliomkuta, wampe heshima anayostahili kwa sababu anao mchango mkubwa sana katika game. 

Ninafahamu kwamba Vicent Kigosi, wakati huo naye akianza kuogelea kwenye umaarufu wa filamu, alikuwa akitoka na dada huyu. Mara kadhaa nimewahi kuwakuta pamoja na kwa maana hiyo, hakuna mdau asiyetambua uhusiano wao. 

Ni kutokana na uhusiano huo, ambao awali ulionekana kama wenye mwelekeo wa kuzaa ndoa, wawili hao walifungua kampuni yao, RJ, kila herufi ikiwakilisha mwanzo wa majina yao ya kisanii.
Lakini kama tunavyofahamu, wawili hawa walianza chokochoko katika uhusiano wao, baada ya kuwepo kwa taarifa za Ray kuchepuka na Chuchu Hans, binti mdogo aliyemkuta Johari katika fani. Mwanzo ilikuwa ni siri, lakini baadaye ikathibitika kuwa ni kweli kiasi kwamba hata Johari akakubali na kumwaga manyanga.
Sijui, labda kwa sababu ni wasichana, wawili hawa wamekuwa wakipigana vijembe kila wanapokaa pamoja au kukutana. Mara moja waliwahi kuripotiwa kupigana katika ofisi za RJ.
Wiki iliyopita, wawili hawa waliripotiwa kutukanana kwa mara nyingine na almanusura wazichape. Walikutana katika eneo ambalo Johari alikuwa ameweka kambi yake, Chuchu akiwa ameambatana na Ray. 

Niseme wazi kuwa ingawa ni vigumu kuzungumzia hisia za watu kimapenzi, lakini kwa uzoefu wa wawili hawa, inaonekana kama wanaishi maisha flani yanayokwenda kinyume na ustaarabu wa kisasa. 

Nianze na Chuchu. Mara zote ugomvi unapotokea, binti huyu huwa amemfuata Ray katika eneo analojua kabisa kuwa Johari atakuwepo, hivi kwa kutumia tu busara zake za kawaida, kwa nini huwa hajiepushi kusogelea? Kwa sababu anajua kuwa yeye alimpora mwenzake mtu wake. 

Hivi anapokwenda ofisini kwa Ray kwa mfano, akijua kabisa Johari pia yupo, haoni kama anayakaribisha matatizo makusudi? Maana yake ni kuwa anakwenda pale akitamba kwamba hawezi kufanywa lolote! 

Na Johari, kwa umri ulionao, huoni kama ni kujifedhehesha tu kumpigania mwanaume unayejua kabisa hana mapenzi nawe? Huhisi watu wanaweza kukuona ni mshamba wa mapenzi?

No comments: