welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 15 October 2014

JIBU LA LULU KWA KIDUME WA KIKONGO ALIYETANGAZA NIA


SiKU chache baada pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu kutangaza kuwa anamtaka staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote, mwigizaji huyo ametoa jibu linaloonesha dhahiri kwamba alikuwa radhi kumkubalia.
Staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’Akizungumza na waandishi wetu mara baada ya habari ya Mkongo huyo kuandikwa gazetini hivi karibuni, Lulu alisema kilichomshangaza kutoka kwa mwanaume huyo ni kwamba hakutakiwa kuanika hisia zake katika vyombo vya habari kama kweli ana nia ya dhati, angemtafuta mwenyewe au kwenda kujitambulisha nyumbani kwao.
“Namshangaa sana huyo Mkongo kwa kweli kama angekuwa na mapenzi ya kweli asingeyaeleza kwenye magazeti, angenitafuta au angekuja nyumbani kwetu hapo ningemuona kweli ananipenda,” alisema Lulu.
Pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu. Staa huyo aliendea kumwaga chache kuwa, kama mwanamke, anahitaji kupewa heshima yake na kudai kuwa wanaume wengi wa sasa wamejisahau kupindishamila za Kiafrika kufuata taratibu na badala yake wanatanguliza fedha mbele.
“Nadhani watu wamesahau mila za Kiafrika kabisa, huwezi kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke halafu utumie rafiki au vyombo vya habari umpate, hiyo inakuwa siyo heshima kabisa,” alisema Lulu.

No comments: