welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Friday 3 October 2014

AIBU! MKE, MUME WAZICHAPA WAFUNGA MTAA

Richard Bukos
Hii ni aibu kubwa! Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu,  Kigogo-Luhanga jijini Dar wamenaswa wakiangusha bonge la timbwili barabarani na kusababisha umati wa watu kujikusanya eneo hilo kujionea ‘sinema’ ya bure.
imbwili zito likianza kati ya njemba mmoja anayefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata.
Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata kilaji.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.Mke akimlia 'taimingi' kumbwaga mume wake kwa mweleka. MUME ATOKA KIDOGO
Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo wa usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi akute msosi uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’Mara Puuuuu...!! wote chini
“Sasa akiwa pale baa, alizidi kunogewa na masaa yalizidi kupotea ndipo Zeno alirudi nyumbani na kukuta mlango umeegeshwa na mkewe hayupo huku akisikia harufu kali ya kitu kuungua na kumfanya apige chafya.
“Alipokaa sawa alibaini kuwa maini aliyoleta yalikuwa yameungua na kuwa kama mkaa hali iliyompandisha hasira na kuanza kumsaka mkewe,” kilidai chanzo hicho.Mume (Bw Zeno) akimburuta mkewe kwa ghadhabu.
AMUIBUKIA BAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, Zeno akiwa katika sakasaka yake ndipo alipombamba mkewe kwenye baa hiyo akimalizia ‘kunyonya’ kilevi kikali.
ZACHAPWA
Bila kuuliza, Zeno alimkunja mkewe na kumtoa nje huku akimpa makofi ndipo Mwajuma akaona kama anaonewa hivyo akamvizia mumewe na kumchota mtama ambapo wote walikwenda chini kutokana na kuwa katika hali ya kuzidiwa na kilaji.Wote wakichukua uamuzi wa kuzima timbwili hilo.
LAHAMIA NJE YA BAA
Timbwili hilo liliendelea nje ya baa hiyo ambapo vijana wawili wa mtaani hapo waliofahamika kwa majina ya Haidani na Kulwa walihofia yangeweza kutokea machafuko zaidi wakakimbilia kwa mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Shukuru lakini walimkuta mke wa mjumbe ambaye aliwaambia mumewe alikuwa kazini.
Mke(Bi Mwajuma Mtata) akijaribu kuzuia kupigwa picha na kamera za wanahabari.
WARUDI NYUMBANI
Wapenzi hao baada ya kugaragazana vya kutosha ikiwa ni pamoja na kuvuana nguo, mwanaume alianza kumburuza mkewe na kurudi nyumbani kwao ambapo walipofika eneo la Kwamkoma walianza kutifuana tena kabla ya kuamuliwa na wasamaria wema.
Jirani akihoji kulikoni mpaka iwe hivi...
ETI WAMEYAMALIZA!
Taarifa tulizozipata wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni juzi, Jumatano, wawili hao walikuwa tayari wameshayamaliza na wanaishi raha mustarehe baada ya kuombana msamaha.

No comments: