welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Friday 26 September 2014

RAIS JK AKIKASIRIKA NYUMBANI KWAKE HUWA INAKUA HIVI.

Labda inawezekana hii ikawa mara yetu ya kwanza kusikia upande wa pili wa President wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae tumezoea tu kumuona akihutubia, akijumuika na watu mbalimbali kwenye matukio ya furaha na huzuni lakini kuna mengine hatuyajui kuhusu yeye.
Mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambae ni mbunge wa Chalinze ameongea kwenye Exclusive na Millard na kueleza ni jinsi gani inavyokua pale ambapo baba yake anakasirika au anapokasirishwa akiwa nyumbani.
‘Jambo akiwa halitaki mara nyingi hupenda kusema achana na hilo lakini kama ni mtu kafanya jambo flani sio zuri utamsikia mzee tu anasema huyu mtu bwana achana nae….. maarifa yake madogo, naweza kutoa ushuhuda mbele za watu mzee wangu mimi sio mtu ambae ameishi kwenye mazingira yanayotoa fursa ya matumizi ya lugha ngumungumu kama matusi‘
‘Yani mtu akimuudhi… huwezi kusikia amefikia hatua ya kutamka labda huyu mshenziiii…. sina kumbukumbu ya mimi kumsikia akitamka neno kama hilo, mara nyingi ukikosea anasema huyu maarifa yake madogo kwelikweli‘ Ridhiwani.

No comments: