welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday 14 September 2014

Masele ambana Kaimu Meneja Tanesco Geita


Geita. Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme (Tanesco) Mkoa wa Geita, wa Geita, Charles Budodi juzi alijikuta kwenye wakati mgumu, baada ya kushindwa kujibu maswali yaliyoelekezwa kwake na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kuhusu shirika hilo kukaidi agizo la Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha shirika hilo linapeleka umeme kwenye shughuli za wachimbaji wadogo.
Hali hiyo ilijitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita, alipowasili kijijini hapo kuzindua mgodi wa mfano wa wachimbaji wadogo. Alipofika eneo hilo, naibu huyo alikuta maeneo ya wachimbaji wadogo hayana huduma ya umeme licha ya umeme kufikishwa katika kijiji hicho,

Masele alionyesha kukerwa na kitendo hicho cha kukaidi agizo la Rais, huku wananchi waliokuwa mkutanoni hapo wakimzomea kaimu meneja huyo kwa kumwomba naibu waziri kuondoka naye wakidai ametoa majibu ya uongo.
Masele.”Meneja yuko wapi…Tuambie kwa nini umeme haujafika kwa wachimbaji wadogo, wakati tayari Rais aliagiza umeme upelekwe huko? Umefanya utafiti ni wachimbaji wangapi wanahitaji umeme”
Meneja, ”Mheshimiwa, tumefanya tathmini na tumezunguka Nyarugusu na hapa Lwamgasa, tutaleta umeme.”

No comments: