welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 10 September 2014

KIFO TATA! ALIYEDAIWA KUUAWA KWA KIPIGO CHA POLISI, UKWELI WAJULIKANA

Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
KIFO cha mfanyabiashara aliyeshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam, Liberatus Damiani Temu (55) kilichodaiwa kilitokana na kipigo kutoka kwa askari wa kituo hicho sasa ukweli umejulikana.

Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Liberatus Damiani Temu (55) anayedaiwa kufariki kiutata. Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa utata wa tukio hilo ulianzia mbali kwani Mei, mwaka huu, marehemu alimgonga na gari mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Hamis Magoma na kujeruhiwa vibaya.
Mke wa marehemu, Naomi Liberatus (katikati) akihuzunika kwa kumpoteza mwenzake.
Baada ya kusababisha ajali hiyo, ilidaiwa marehemu Liberatus alifuatilia masuala ya bima ili aweze kumlipa aliyemgonga ambaye pia anatajwa kuwa mteja mzuri katika Baa ya Meku iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu.Naomi Liberatus akiwa amezimia wakati wa mazishi. Chanzo kinasema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, hali ya Magoma iliendelea kuwa mbaya hadi Agosti 22, mwaka huu saa tano usiku marehemu alipokamatwa na kufikishwa kituoni hapo akidaiwa kumjeruhi Magoma kwenye ajali.Padri akiiombea roho ya marehemu ya marehemu (Liberatus Damiani Temu). Mke wa marehemu, Naomi Liberatus aliyezimia mara mbili wakati wa mazishi, alisema mumewe ambaye kwa kipindi chote tangu apate ajali hiyo, alikuwa hafanyi shughuli yoyote, alikataliwa kupewa dhamana kwa madai kuwa majeruhi (Magoma) alikuwa na hali mbaya.Mwili wa marehemu Liberatus Damiani Temu ukichukuliwa kwenye gari kwa ajili ya mazishi. Kuhusu hatua nyingine ilidaiwa kuwa marehemu akiwa mahabusu aligonga kichwa chake kwa nguvu ukutani, hali iliyosababisha wenzake kupiga kelele za kuomba msaada na kwamba baada ya askari kufika na kukuta hali ilivyo, walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu ambako alifariki dunia.Marehemu Liberatus Damiani Temu enzi za uhai wake.
“Watu wanasemasema tu kwamba Liberatus aliuawa na askari, si kweli. Kwa nini tumuue? Kwa kosa lipi? Sisi tulimshikilia kwa sababu hali ya majeruhi aliyemgonga ilikuwa mbaya, hivyo kumweka mahabusu marehemu ilikuwa kwa ajili ya usalama wake pia.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua jambo. “Wengi wanaamini kila anayewekwa mahabusu ni mhalifu wa kiwango cha kuteswa na polisi, si kweli. Wengine wanakaa hapa ili kuwalinda. Wewe ukiua unadhani ndugu wa marehemu watakuacha?” alisema askari mmoja wa kituo hicho bila kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji mkuu.
Alisema kuwa mahabusu waliokuwa na marehemu ni mashahidi wakubwa kwamba jamaa alijigonga kichwa ukutani lakini kabla ya kufanya hivyo, alikuwa akisemasema maneno mengi kama aliyechanganyikiwa.

Hata hivyo, marehemu amezikwa akiacha maswali kibao, watu wanajiuliza je, kilichosemwa na polisi ndiyo ukweli au la! Kufuatia utata wa kifo hicho, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameunda tume kufuatilia sakata hilo.

No comments: