welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday 21 September 2014

MLIPUKO WAUA MAOFISA WA POLISI MISRI

Maofisa wa polisi wakiwa eneo ulipotokea mlipuko huo.
MAOFISA wawili wa polisi wameuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea leo kwenye wilaya ya Bulaq Abu-al-Ila jirani na Wizara ya Mambo ya Nje jijini Cairo nchini Misri.
Mlipuko huo umetokea katika mtaa uliojaa watu wengi jirani na Mto Nile na bomu hilo linadaiwa kutegwa chini ya mti uliokuwa katika eneo hilo.
Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo.
Tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Mohammed Morsi, Julai mwaka jana, Misri imekuwa ikishuhudia misururu ya milipuko na mashambulizi yanayowalenga maafisa wa polisi na wanajeshi.

No comments: