Staa wa filamu Bongo Jacqueline Wolper Massawe akisalimiana na Sista wa Kanisa Katoliki la Msimbazi, jijini Dar.
STAA Jacqueline Wolper Massawe, ambaye ni muigizaji mahiri wa filamu,
amewapiku nyota wenzake wa tasnia hiyo baada ya kufanya kumbukumbu ya
siku yake ya kuzaliwa Jumamosi iliyopita kwa namna tofauti kabisa, kwani
badala ya kuita marafiki kwenye pati kubwa inayoambatana na vyakula na
vinywaji, yeye alikwenda kuwatembelea wazee wanaolelewa katika Kanisa
Katoliki la Msimbazi, jijini Dar.
Katika kituo hicho kinachowalea wazee wa kike na kiume, Wolper
aliyeambatana na rafiki yake Kajala Masanja na wale aliowatambulisha
kama Wolper Family, muigizaji huyo alitoa zawadi ya mchele mifuko miwili
ya kilo 50 kila moja, sukari mifuko miwili ya kilo 50, sembe kilo 50
pia, sambamba na mafuta ya kupikia madumu mawili, vitu ambavyo alikataa
kutaja thamani yake.
Wolper Massawe akitoa zawadi katika kituo cha kulelea wazee cha Kanisa Katoliki cha Msimbazi.
“Siku hizi nimekuwa mtu mzima, nimeachana na mambo ya sherehe kwa
sababu nimeona ninakuwa napoteza pesa kwa mambo yasiyo ya muhimu, ni
jambo la heri kwangu kuwasaidia wazee kwani nawapenda na naamini hata
wao wanatupa sapoti kubwa sana kwenye kazi zetu, japo kuna watu
walitarajia waone nini kitafanyika kwenye siku yangu hii ya kuzaliwa
kuhusu sherehe,”alisema Wolper.
Wazee wakimshukuru Wolper Massawe kwa upendo aliouonyesha kwao.
Marafiki zake kutoka Wolper Family walisema ni wao ndiyo waliomshauri
staa huyo kufanya kitu hicho ili kuwa tofauti na wenzake ambao
kumbukumbu ya kuzaliwa kwao hufanywa kwa matumizi makubwa ya fedha
yasiyo ya lazima.
Wolper
akipozi pichani na shosti yake Kajala. “Alitaka kufanya sherehe
tukamshauri aachane na hilo suala tuliona atapoteza pesa kwa sababu
angefanya sherehe watu wangekunywa pombe, wangevaa vinguo vya ajabu,
kitu ambacho ni kama laana kwake, badala yake kwa hili alilolifanya
atapata baraka na mambo yake yatamnyookea,” alisema mmoja wa mashabiki
wake kutoka Wolper Family.
Baada ya kukabidhi msaada wa vyakula hivyo, mmoja wa wazee hao Bibi
Rachel Christopher, alimpa somo Wolper kuwa ni vema wakaishi vizuri na
mashabiki wao na kuachana na mavazi ya ajabu kwani yanawashushia hadhi
zao.Wolper
akiwa katika picha ya pamoja na Wolper Family.“Mimi huwa naangalia sana
filamu zao, ninawapenda na huyu leo katimiza miaka kadhaa tangu
kuzaliwa kwake, tunamuombea uzima, afya tele na maisha marefu,” alisema
bibi huyo ambaye pia aliwataka waigizaji wa kiume na wasanii kuacha
kuvaa suruali kwa mtindo wa kata K.
No comments:
Post a Comment