SENTENSI ALIZOZIONGEA MUME WA LADY JAY DEE, GADNER HABASH KWENYE MKASI!
Mtangazaji
Gardner G. Habash ni miongoni mwa Watangazaji hodari ambao Tanzania
imewahi kuwa nao ambapo alianza kwa kusikika kupitia CloudsFM kwenye
shows mbalimbali ikiwemo Jahazi kabla ya kuanza kazi.Wakati huu ambapo
kumekua na stori zilizoenea mtaani kuhusu yeye na ndoa yake pia kazi,
show ya TV ya Mkasi inayoongozwa na mtangazaji Salama Jabir imepata
nafasi Exclusive ya kuongea nae. Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya
sentensi alizoziongea Captain G kwenye Mkasi on EATV. Kwanza
alianza kwa kuongelea jinsi alivyoingia kufanya kazi Redioni
hukuakimkumbuka Othman Njaidi aliemchukua na kumpeleka CloudsFM sio kama
mtangazaji bali akajiunge na timu ya Marketing, akakutanishwa na Ruge
Mutahaba aliekua General Manager wakati huo ambae alipoisikia tu lafudhi
ya Gardner akasema huyu anafaa kuwa mtangazaji. Staa aliefurahi baada ya kukutana nae ni D’Banj wa Nigeria, alifurahia uchangamfu wake…
Salama
alipomuuliza kuhusu uhodari wake wa kutangaza habari za mastaa wa
dunia… Captain G. akasema ‘nilikua nanunua majarida kwenye maduka
yanayouza majarida kutoka nje, wakati Internet hamna kulikua na majarida
mengi kidogo’
‘Mimi ni mchaga kabisa wa Baba na Mama lakini
Wazazi wangu walihamia Tanga zamani alafu mimi nimezaliwa Ngamiani pale
Hospitali na tukaishi Chumbageni muda mrefu kwa hiyo nilipata lafudhi ya
Tanga pale, na hiyohiyo lafudhi ya Tanga ndio iliyonipa kazi kwenye
Radio’
Salama akamuuliza ‘Unajisikiaje ukisikia mtu anatangaza
kama wewe‘ >> Gardner akajibu ‘kuna baadhi ya watu kusema ukweli
wanachukizwa sana na hicho kitu na wananilalamikia sana kwamba kuna
Watangazaji wengi wamekua wanakuiga kwenye kutangaza Redioni na kwenye
kutengeneza jingle kama za kwako lakini mimi nimeiona ni baraka kwangu,
kama watu wamekupenda kiasi kwamba wanakuiga ni jambo la kufurahisha
kwangu mimi linanifurahisha sana’
Kuhusu kitu kilichomfanya
akaondoka kwenye Radio, Captain amesema ‘Nilifanya kazi miaka 9 akili
ikawa imechoka nikafikiria lazima pia nifanye biashara watu wanakusifia
kwamba una uhodari flani kwa hiyo unajipa challenge kwanini
nisitengeneze kitu changu, ndio tukafungua biashara za chakula lakini
zaidi nilikua nataka kupumzika’
Swali jingine kutoka kwa Salama
likawa ‘nasikia kuna stori kwamba hivi karibuni pia unaweza kurudi kule
ama ukaenda sehemu nyingine‘ Captain G. akajibu >>> ‘ni mmoja
kati ya hao wawili, stori ni ya ukweli ndio maana naondoka, nimemaliza
mkataba nimepata ofa nyingine kubwa naichukua’
Swali jingine
lililokua linasubiriwa ni hili alilouliza Salama >> ‘kuna stori
mtaani kwamba wewe na Lady Jaydee mmeachana’ Gardner akajibu ‘mimi
sijawahi kupata interview muda mrefu sana… nadhani hii inaweza kuwa
interview yangu ya kwanza, kwahiyo nilikua nataka nikuombe tuongee
kuhusu mimi kwanza manake tukizungumzia kuhusu JayDee nitafunikwa hapa’
No comments:
Post a Comment