MAOFISA
wa Polisi, Uhamiaji pamoja na Mahakimu watashiriki kwenye semina ya
Siku Ya Msanii Tanzania itakayofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho
‘Mwalimu Nyerere’ Posta, Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari
(Maelezo), Katibu Mkuu wa Mashirikisho Tanzania Godfrey Ndimbo alisema
wamewaita watu kutoka sekta hiyo ya sheria ili kujua tatizo la wizi wa
kazi za wasanii likoje.
“Tumewaita
mahakimu, Polisi na Uhamiaji ili waweze kujua hasa ukubwa wa tatizo
letu, tukishirikiana nao watakuwa msaada mkubwa kwetu katika kupambana
na wizi wa kazi za sanaa.
“Katika
semina hizi pia tutakuwa na waandishi wa habari ambao watasaidia pia
kufikisha ujumbe kwa jamii katika kupambana na wizi wowote wa kazi za
wasanii,” alisema.
Ndimbo
alisema katika semina hizo zitakazofanyika Oktoba 22 na 23,
zitajumuisha pia elimu kuhusu haki miliki na haki shiriki, kodi, bima za
afya pamoja na mifuko ya Jamii.Mkurugenzi wa Haak Neel Production,
Godfrey Katula alisema maandalizi kwa ajili ya semina hizo yanakwenda
vizuri na wanatarajia wasanii zaidi ya 500 kushiriki kwenye semina hizo.
“Lengo
letu ni kuwaelimisha wasanii katika kazi zao, lakini pia kuweza
kuwapana nafasi ya kupata mafunzo yatakayowasaidia uzeeni wakati ambapo
hawatakuwa wakifanya tena sanaa,” alisema.
Siku
Ya Msanii inaandaliwa na Kampuni ya Haak Neel Production kwa
kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kudhaminiwa na
Kampuni ya New Habari (2006) kupitia magazeti ya Bingwa, Dimba, The
African na Mtanzania, PSPF, Hugho Domingo, Afrika Media Group kupitia
Channel Ten na Magic FM, CXC na Proin Tanzania.
No comments:
Post a Comment