Ajira
imekua gumzo kila sehemu uendapo nchini kwetu hata pia nchi
nyingine.wasomi kwa wasiokua wasomi pasenti kubwa wanapitia tatizo
hili.tatizo la ajira limevunja myoyo ya wengi na wengine kukata tamaa na
kuamua kufanya vitu wasingefanya ili kuweza kujipatia riziki na chakula
cha kila siku. Tatizo hili limesababisha mauaji na upotezi wa maisha ya
vijana bila hatia na pia kuongeza uhalifu na pia wengine kujiingiza
katika mambo tofauti ili kuepuka umaskini. Wanaotafuta kazi ni wengi
kuliko wanaotafuta wafanyakazi nah ii umesababisha mashindano makazini
na maofisini.
Kinachoshangaza
wasio na kazi ni wale ambao wamemaliza masomo yao.tatizo tulilanao kama
vijana wa kitanzania ni kua na dharau ya kazi.tunapenda kufanya kujenga
jina na sio maisha yetu au kujifunza zaidi na kwasababu ya hili wengi
wametupita katika maisha. Hivyo nasimama katika nafasi ya vijana
wenzangu kutoa ushauri kwa wenzangu ambao bado mnategemea kazi.chochote
chema ambacho unaweza fanya ili kujipatia kipato kifanye na usiangalie
watu watasemaje kwasababu hao hao utakapoanza kufanikiwa kifedha
watakuja kuchukua mikopo na tusipende kuiga wengine wanachofanya ili
nasisi tufanye kama wao.tunaweza tukapambana na tatizo hili kama
tutajishusha na kutoa vibuli katika maisha yetu ili tukubali uharisia wa
maisha kwasababu ni bora kua na hicho kidogo kuliko kukosa kabisa na
kwakusema hivyo sisemi kwamba msiwaze makubwa bali nashauri kwamba
tuende kwa hatua katika kila tulifanyalo ili tusijikwae mbele ya safari
yetu ya mafanikio.vijana tuna nguvu na tuitumie katika mema yakufuraisha
na pia kuendeleza waliotuzunguka na kwa uhai Mungu aliotupa bado
matumaini yapo.tumtangulize Mungu mbele katika kila jambo nae
atatusaidia katika maisha yetu pia.
Kwa mawasiliano zaidi
0688440029
instagram:ellydavid
No comments:
Post a Comment