. BW.WILIAM MUSHI (32),aliyemwagiwa maji ya moto na mke wake,tunu kimaroTukio hilo la kikatili lilitokea Agosti 15, mwaka huu nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam na lilishangaza majirani kutokana na Tunu kudaiwa kuchukuwa maji ya moto yaliyokuwa yanachemka na kuwamwagia bila huruma.
CHANZO NI MTOTO
Akisumulia mkasa huo Mushi alikuwa na haya ya kusema:
“Mke wangu anaitwa Tunu Kimaro ana miaka 23. Alinimwagia maji ya moto baada ya kumkuta mwanangu wa miezi saba hali yake ya kiafya ikiwa siyo nzuri, nilipokuwa naondoka asubuhi nilimuagiza ampeleke hospitali.
Mtoto mchanga wa bw wiliam mushi aliyeunguzwa pia na maji ya moto“Baada
ya kufika nyumbani na kumkuta mwanagu Ivan amenyong’onyea,
nilipomuuliza mke wangu sababu za kutompeleka hospitali alinijibu majibu
ya kijeuri kama siyo mke wangu na mtoto siyo wake.
“Niliendelea kumtaka anieleze sababu ya kutompeleka mtoto wetu hospitali ndipo aliposema ngoja anioneshe.
“Alitoka
nje kumbe alikuwa anachemsha maji, alikuja nayo yakiwa kwenye sufuria
aliloshika kwa kitambaa, akatumwagia mimi na mwanangu ambaye anajua
hajui chochote,” alisema Mushi.“Niliendelea kumtaka anieleze sababu ya kutompeleka mtoto wetu hospitali ndipo aliposema ngoja anioneshe.
LENGO LAKE KUTUUA
Akaongeza: “Naamini lengo lake lilikuwa ni kutuua na si vinginevyo. Ni jambo la kusikitisha sana na majirani nao walisoneneshwa na tukio hili baya.
“Ni vyema angesubiri niwe peke yangu, lakini alitumwagia maji akijua kuwa nina mtoto tena mchanga. Nashukuru Mungu kwa sababu nilijitahidi kumkwepesha na maji yale ya moto, lakini yalimpata na kumuunguza kama unavyoona.”
AKIMBILIA POLISI
Mume huyo alisema: “Baada ya mke wangu kutufanyia kitendo kile alikimbilia polisi na kudai eti kuna mtu amemshambulia.
“lakini baadaye nilipopelekwa polisi kuchukua PF 3 (hati ya kuruhusu nitibiwe), askari walishangaa kuona nilivyounguzwa mimi na mwanangu na walipigwa na butwaa nilipowaeleza kuwa aliyefanya hivyo ni mke wangu.
“Askari polisi baada ya kupata ukweli ilibidi mke wangu awekwe ndani ili aweze kutoa maelelezo ilikuwaje. Nashindwa kuelewa kama sababu ni kumlaumu kwa kutompeleka hosptali mtoto wetu au kuna jambo lingine.
“Nahisi kuna mtu anamtia kiburi kwa sababu mke wangu hakuwa na tabia hizi za kujibu kijeuri na moyo wa kikatili, watu wengine walidhani huyu mtoto yupo kwa mama wa kambo,” alisema Mushi.
Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mtoto amelazwa katika kitengo cha watoto walioungua.
AFISA WA POLISI ANENA
Mama wa mtoto huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Urafiki, jijini Dar es Salaam ambapo afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwa kuwa siyo msemaji alisema upelelezi ukikamilika ni lazima sheria ichukue mkondo wake.
MUUGUZI ANASEMAJE?
Muuguzi aliyekuwa zamu siku hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Cristene Chilambo, alishangazwa na kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo na kuongeza kuwa hali ya mtoto inaendelea vizuri.
“Mtoto huyu hana kosa lolote, mama yake amekosea sana na naomba taasisi za haki za binadamu zifanyie kazi ukatili huu maana huu ni unyama na ukatili wa aina yake,” alisema Chilambo.
No comments:
Post a Comment