welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Tuesday 7 October 2014

PROIN PROMOTIONS YADHAMINI SIKU YA MSANII TANZANIA

MAOFISA wa Polisi, Uhamiaji pamoja na Mahakimu watashiriki kwenye semina ya Siku Ya Msanii Tanzania itakayofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ‘Mwalimu Nyerere’ Posta, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),  Katibu Mkuu wa Mashirikisho Tanzania Godfrey Ndimbo alisema wamewaita watu kutoka sekta hiyo ya sheria ili kujua tatizo la wizi wa kazi za wasanii likoje.

“Tumewaita mahakimu, Polisi na Uhamiaji ili waweze kujua hasa ukubwa wa tatizo letu, tukishirikiana nao watakuwa msaada mkubwa kwetu katika kupambana na wizi wa kazi za sanaa.

“Katika semina hizi pia tutakuwa na waandishi wa habari ambao watasaidia pia kufikisha ujumbe kwa jamii katika kupambana na wizi wowote wa kazi za wasanii,” alisema.

Ndimbo alisema katika semina hizo zitakazofanyika Oktoba 22 na 23, zitajumuisha pia elimu kuhusu haki miliki na haki shiriki, kodi, bima za afya pamoja na mifuko ya Jamii.Mkurugenzi wa Haak Neel Production, Godfrey Katula alisema maandalizi kwa ajili ya semina hizo yanakwenda vizuri na wanatarajia wasanii zaidi ya 500 kushiriki kwenye semina hizo.

“Lengo letu ni kuwaelimisha wasanii katika kazi zao, lakini pia kuweza kuwapana nafasi ya kupata mafunzo yatakayowasaidia uzeeni wakati ambapo hawatakuwa wakifanya tena sanaa,” alisema.

Siku Ya Msanii inaandaliwa na Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kudhaminiwa na Kampuni ya New Habari (2006) kupitia magazeti ya Bingwa, Dimba, The African na Mtanzania, PSPF, Hugho Domingo, Afrika Media Group kupitia Channel Ten na Magic FM, CXC na Proin Tanzania.

No comments: