welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday 12 October 2014

NYOTA WA BENIN WATUA DAR


Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti. Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg, Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).

 Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
 Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).
 Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo (Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni.
Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.
FDL YAANZA KUTIMUA VUMBI
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015 inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 11 mwaka huu) katika viwanja tisa tofauti kwenye miji ya Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza, Geita, Mbozi, Songea, Mufindi na Dar es Salaam.
 Kundi A litakuwa na mechi kati ya Kimondo FC na Villa Squad itachezwa Uwanja wa Vwawa mjini Mbozi wakati Majimaji itaumana na Ashanti United (Uwanja wa Majimaji, Songea).
 Nyingine ni Kurugenzi Mafinga na Tessema FC kwenye Uwanja wa Mufindi huku Friends Rangers ikioneshana kazi na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
 Kundi B ni Panone itaikabili Kanembwa JKT (Uwanja wa Ushirika, Moshi), Oljoro JKT itapambana na Polisi Dodoma (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abedi, Arusha), Polisi Mara na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Musoma).
 Mechi nyingine ni kati ya Toto Africans na Mwadui itakayofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Geita Gold na Burkina Faso (Uwanja wa Waja, Geita).
 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments: