welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday 23 October 2014

NEWS : ALIYEPIGWA RISASI AFARIKI DUNIA


Nyakiringa Stivin (39), mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mkewe, Agness Lucas.
....wapita njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.Global Publishers jana ilikuwa ya kwanza kuripoti tukio la mwanamme mmoja kupigwa risasi maeneo ya Magomeni Mikumi ambaye hakuweza kutambulika mara moja, lakini sasa amejulikana na kwa taarifa zilizotolewa na ndugu, jamaa huyo amefariki dunia leo afajiri akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Marehemu ametambulika kwa jina la Nyakiringa Stivin (39), mkazi wa Kibaha Picha ya Ndege na mwanamke aliyekuwa naye kwenye gari ameelezwa kuwa ni mkewe, Agness Lucas. Marehemu ni fundi wa sofa na imeelezwa na chanzo chetu kuwa alikuja jijini Dar kwa ajili ya kununua mahitaji yake ya ufundi.
Alipopigwa risasi maeneo ya Magomeni alikuwa akitokea Access Bank Manzese ambako alitoa fedha kiasi cha shilingi 12M. Kwa mujibu wa mkewe, mkoba uliochukuliwa na majambazi ulikuwa na shilingi milioni 10 ambazo zilibaki baada ya kufanya manunuzi maeneo ya Manzese.

No comments: