welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday 12 October 2014

MCHECHU AONGOZA HAFLA YA KUCHANGIA VITABU 2500 KWA SHULE ZA SEKONDARI NA ZA MSINGI ILIYOANDALIWA NA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI YA NKWAMIRA

 Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akihutubia wakati wa hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam  ya Shirika Lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Nkwamira Sustainable Life Trust, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 10, 2014 jijini Dar es Salaam. NHC imechangia kiasi cha shilingi milioni 12, na imeahidi kujenga madarasa mawili katika shule ya msingi Saku iliyopo Mbagala. 

Azim Jamal ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc kampuni inayojishughulisha na kusaidia wadau  na makampuni kupata stahiki katika kazi zao,na ni mwandishi wa vitabu mbalimbali vilivyotafsiriwa katika lugha 10, akizungumza katika hafla hiyo jana.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Madini nchini, Richard Kasesela akizungumza wakati wa hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,  ya Shirika Lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Nkwamira Sustainable Life Trust
 Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo
Muongozaji wa sherehe hiyo maarufu kama MC Luvanda, Anthony Luvanda akiinua picha juu kuinadi kwenye hafla hiyo ya uchangiaji kwaajili ya kuwezesha watoto kupata vitabu vya kusoma.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari akifuatilia jambo katika hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Omari Mjenga kwenye hafla hiyo.
 Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo
 Wadau Abdul Njaidi na mwenzie wakifuatilia jambo katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Saku wakitoa ushuhuda wao wa namna wanavyopata shida kupata elimu katika shule yao hiyo ambapo walisema wengi wao wanakaa chini na vitabu na madarasa hayatoshi.
 Kikundi cha burudani cha Dar Choral Society wakitumbuiza muziki laini katika hafla hiyo jioni ya jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Kikundi cha burudani cha Dar Choral Society wakitumbuiza katika hafla hiyo jioni ya jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Kikundi cha burudani cha Dar Choral Society wakitumbuiza katika hafla hiyo jioni ya jana kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), William Genya, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari na Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu, Veronica Mtemi wakifuatilia hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Nehemia Kyando Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla wakifuatilia hafla hiyo
Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo.
 Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipokea hundi ya Shilingi milioni saba iliyotolewa na Benki ya KCB jana jioni.
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipokea hundi ya Shilingi milioni saba iliyotolewa na Benki ya KCB jana jioni.

No comments: