welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Friday 10 October 2014

DUNIA INA MAMBO: WANAFUNZI WASHAURIWA KUJISAIDIA BAFUNI WAKATI WAKUOGA


Wanafunzi walioanzisha mradi huo Debs Torr na Chris DobsonWanafunzi wa vyo vikuu nchini Uingereza wametakiwa kwenda haja ndogo bafuni katika juhudi za kuzuia matumizi mabaya ya maji.Kampeni yenye kauli mbiu, 'Go with the Flow' ilianzishwa na wanafunzi na wawili wa chuo kikuu cha East Anglia mjini Norwich.
Wanafunzi hao Debs Torr na Chris Dobson wanataka chuo hicho chenye wanafunci 15,000 kwenda haja ndogo wakiwa wanaoga asubuhi na mapema.


Mwanafunzi Dobson, mwenye umri wa miaka 20, alisema kwamba wazo hilo litaokoa matumizi ya maji na kujaza bwawa la kuogelea la chuo hicho ambalo lina uhaba wa maji.
Bwawa lenyewe ni kubwa sawa la bwawa linalotumiwa kwa mashindano ya olimpiki.
Wanafunzi walioanzisha kampeini hiyo wanawataka wenzao kuahidi kwenye Facebook na Twitter na pia kuahidi kuwazawadi wanafunzi wa kwanza kufanya hivyo.
Wanasema hakuna taisho ya watu kupata maradhi
Dobson amesema :"tumefanya uchunguzi wetu na mradi huu utakuwa na matokeo mazuri sana. ''
"wanafunzi wote hawa ikiwa watafanya hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, watazuia uharibifu wa maji na itatusaidia kujaza bwawa letu mara 26. ''

"tunajitahidi kubadili tabia na mienendo ya wanafunzi wenzetu, kuanzisha mjadala kuhusu maji, rasilimali ambayo sisi hupuuza sana umuhimu wake.''

Dobson alisema kuwa walitoa ushauri wao kwa profesa mmoja na pia kufanya uchunguzi wao wenyewe kuhusu tisho lolote kwa afya ya watu wanaotumia bafu moja.

No comments: