welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday 16 October 2014

AUNT EZEKIEL NAYE AFUNGUKA KUHUSU KU-SPEND NA MH. WAZIRI NCHINI MAREKANI!


Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel . 
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu nchini Marekani, kwani alikutana naye ukumbini, akiwa amealikwa na blog iitwayo Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa Tanzania nchini humo kila mwaka.Alisema wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu Waziri Nyalandu na anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada ya kumsalimia walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea, kwani yeye alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa shughuli hiyo ulipokuwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo. “Watu wanataka kunijengea uadui na mke wake Faraja Kota ambaye tunaheshimiana sana, mimi nilialikwa kule nikiwa na wasanii wengine, wanamuziki Kassim Mganga na IT na hata malipo ya kazi yangu nililipwa na wao, wanaosema nilitumia hela za wizara sijui wanataka nini, kama wizara iliwapa fedha hao waliotualika mimi sijui,” alisema muigizaji huyo.

No comments: