welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday 16 October 2014

ANGALIA PICHA GARI LILILOBEBA NG’OMBE LAPATA AJALI UBUNGO DAR

Mfanyabiashara wa mifugo hiyo, Abdalah Juma, akionyesha eneo la bega aliloumia katika ajali. 
Gari lilivyokuwa baada ya ajali.Mifugo ikiwa kando ya barabara baada ya ajali.Eneo ajali ilipotokea. MFANYABIASHARA mmoja wa mifugo (ng’ombe) na dereva waliokuwa katika lori lililokuwa limebeba mifugo hiyo, leo wamenusurika katika ajali iliyotokea asubuhi eneo la Ubungo-Mataa, jijini Dar es Salaam.
Gari hilo lililokuwa limebeba ng’ombe wapatao thelathini likitokea Wilayani Kondoa, Dodoma, limepata ajali na ng’ombe kadhaa kuumia sehemu mbalimbali za miili .
Wakizungumza na mtandao huu, mashuhuda wamesema tukio hilo lilifuatia mwendesha pikipiki (bodaboda) kukatiza kwa kasi mbele ya gari hilo na dereva alipoamua kuwakwepa, gari lilianguka.
Aidha mfanyabiashara wa mifugo hiyo, Abdalah Juma, amelipongeza jeshi la polisi na askari kwa ulinzi walioufanya hapo kwani hakuna kitu kilichopotea.

No comments: