welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday 14 September 2014

Bunge Maalumu lilivyowavuruga Wanahabari


Bunge Maalumu la Katiba linaeelekea ukingoni.Yapo mambo mengi yaliyofanywa kuhusu Mchakato wa Katiba ndani na nje ya Bunge hilo.
Mathalani katika shughuli za Bunge kulikuwa na idara na taasisi kadhaa ambazo bila ya uwepo wake kazi nzima isingeweza kufikia mahali hapa sasa.
Miongoni mwa idara hizo ni Habari na Itifaki ambayo kazi yake kubwa ndani ya bunge hilo ilikuwa ni kufanya shughuli zote za uratibu wa namna habari za bunge hilo zitakavyowafikia wananchi.

Vyombo mbalimbali vya habari vilituma wawakilishi wao katika Bunge hili ambao wamefanya kazi ya kupeleka kwa jamii kila kilichotokea ndani ya jengo hilo licha ya kuwa baadhi ya mambo watawala waliyapinga.
Oweni Mwandumbya ni mtumishi wa Bunge katika idara ya Habari na Itifaki ambaye wakati wote amekuwa karibu na vyombo vya habari na wanahabari katika kuhakikisha shughuli zao zinafanikiwa.
Akiwa ofisini kwake anazungumzia namna ambavyo kazi hiyo ilikuwa na msisimko mkubwa na jinsi jamii na wanahabari walivyomfanya akose usingizi wakati wote. Fuatilia mahojiano yake hayo na gazeti na gazeti hili:
Swali: Idara ya habari mmekuwa ni sehemu ya bunge hili, lakini muda mwingi hamuonekani kabisa na mnapoonekana ni pale ambapo mnabebeshwa lawama, nini mchango wenu?
Jibu: Ni kweli, unaweza kuona kama hatupo vile lakini ukweli ni kuwa bila ya idara hii pamoja na wanahabari wake, Watanzania walio wengi wasingeona kila kinachoendelea.
Swali: Kazi yenu ni nini hasa katika Bunge la Katiba?
Jibu: Kazi yetu ni kuratibu, kusimamia na kushughulikia masuala yote ya habari za Bunge la Katiba na kuhakikisha tunafikisha ujumbe kwa jamii.
Kazi nyingine ni kuweka mazingira ambayo yatamwezesha mwandishi wa habari wa Bunge la Katiba kufanya kazi yake kwa ufanisi bila wasiwasi.
Swali: Nani ni mwandishi wa habari za Bunge maalumu a Katiba, au kila mtu anaweza kuandika habari za Bunge hili?

No comments: