welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Monday, 1 December 2014

DIAMOND.MAMA'KE ZARI WALA BATA SAUZ


Mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akila bata na mtoto mzuri, ‘Zari The Boss Lady’.
GOOD time! Katika hali ya kushangaza, mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama’ke (Sanura Kassim ‘Sandra’) na mama la mama, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamekutana pande za Sauz na kuponda raha, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.Chanzo makini kilicho karibu na Diamond, kimeeleza kuwa msanii huyo na mama’ke, katikati ya wiki iliyopita, walikwea ‘pipa’ kwenda nchini humo kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuhudhuria ‘event’ ya utoaji Tuzo za Channel O (Choamva) ambazo msanii huyo ameshiriki.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Zari wkiwa kwenye picha ya pamoja na Kampani waliyokuwa nayo Sauzi.

Kwenye tuzo hizo, Diamond ameingia katika vipengele vinne tofauti; Video Bora ya Mwaka, Mwanamuziki Bora Chipukizi, Mwanamuziki Bora wa Afro Pop na Mwanamuziki Bora wa Afrika Mashariki.
Chanzo hicho kilisema pamoja na event ya tuzo hizo, Diamond atatumia muda huo kukutana na mtoto mzuri Zari ambaye ndiye anayedaiwa kurithi mikoba ya aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu ‘Madam’ waliyemwagana hivi karibuni.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipozi na mama’ke (Sanura Kassim ‘Sandra’).
“Diamond ameona bora aondoke na mama’ke wakale bata lakini pia watakutana na wifi Zari si unajua tena ndiyo kwanza mahaba niue…project zinaendelea Sauz,” kilisema chanzo hicho makini.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kuwasiliana na Diamond ambaye pia aliambatana na dada’ke wa hiyari, Halima Kimwana lakini hakuwa tayari kuzungumzia chochote juu ya ukaribu wake na Zari zaidi ya kuanika picha zilizomuonesha akiponda raha.

No comments: