welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 26 November 2014

UTATA MTUPU: DK CHENI ALISHWA SUMU TENA!

Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ akiwa hoi hospitalini.Akizungumza na mwandishi wetu wikiendi iliyopita Dk Cheni alisema kuwa alikuwa mshehereshaji (MC) kwenye harusi moja iliyofanyika maeneo ya Sinza jijini Dar ndipo akala chakula hicho ambapo muda mfupi baadaye alianza kujisikia vibaya ‘kichina’.


Staa wa kiume wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, kwa mara nyingine alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar baada ya kudaiwa kula chakula kinachosadikika kuwa na sumu (poisonous food).

Staa huyo alisema kuwa baada ya hatua chache kutoka ukumbini, tumbo lilianza kumuuma kisha akaishiwa nguvu ndipo akaweka gari pembeni na kupiga simu kwa ndugu kuomba msaada.Dk Cheni aliendelea kueleza kuwa baada ya kupata msaada moja kwa moja alipelekwa kwenye Hospitali ya Burhani jijini Dar.

No comments: