welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 12 November 2014

UTATA MTUPU! DENTE AFAULU APOTEA JIJINI DAR


Mwanafunzi Asia Hamed Muagi aliyepotea katika mazingira tatanishi . Akizungumza na gazeti hili, mjomba wa mwanafunzi huyo ambaye matokeo ya darasa la saba yanaonyesha amefaulu kwa masomo ya sekondari, Mbaraka Mohamed alisema binti yao aliondoka kuelekea kusikojulikana na wamefanya jitihada zote za kumtafuta bila mafanikio. 
MWANAFUNZI Asia Hamed Muagi (15) ambaye alifanya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Gerezani jijini Dar es Salaam amepotea katika mazingira ya kutatanisha tokea Oktoba 28.
Baada ya kumsaka kila kona, tulienda kutoa taarifa kituo cha polisi Msimbazi ambako tulifunguliwa jalada lenye kumbukumbu na Ms/RB/10027.2014 taarifa ya kupotelewa na mtoto,” alisema. 
Asia, mkazi wa mtaa wa Lindi, Kariakoo jijini Dar es Salaam hajaonekana kwa ndugu na marafiki wote wa familia, hivyo mjomba wake anaomba yeyote mwenye taarifa zake kutoa ripoti polisi au kuwasiliana naye kwa namba 0713 400423, 0712 294191 au 07134 480002.

No comments: