welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 26 November 2014

MTOTO MWENYE ULEMAVU ABAKWA NA KUAMBUKIZWA MAGONJWA YA NGONO HUKO MBAYA


Mtoto mlemavu wa akili na miguu mwenye miaka14 anadaiwa kubakwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa na mwanaume mwenye umri wa miaka50.

Mwanaume huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho siku moja kabla ya kufunga ndoa na mke mpya aliyemlipia mahari eneo la Uyole Mbeya baada ya kuachana na mke wake wa kwanza aliyezaa naye watoto zaidi ya watatu.

Tukio hilo lilitokea November 4 na kuripotiwa kituo cha polisi ambapo mpaka sasa mtuhumiwa anasakwa na polisi kwa ajili ya ufunguliwa kesi ya kubaka.

Shangazi wa mtoto huyo akizungumza kwa masikitiko alisema waligundua mtoto wao amefanyiwa kitendo hicho baada ya kutoka kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo huku akilia na walipomchunguza ndipo walipobaini kuwa amebakwa na vipimo vilionyesha ameambukizwa magonjwa ya zinaa.

No comments: