welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 26 November 2014

MAZISHI YA BILIONEA WA MAPENZI GARINI BUKOBA HISTORIA

Msafara wa magari kuelekea kwenye mazishi. Tukio hilo la mazishi lilijiri Jumamosi iliyopita katika Kijiji cha Kyaikailabwa, nje kidogo ya mji wa Bukoba ambapo siku hiyo, shughuli zote zilisimama kwa siku nzima kupisha tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi.


ACHANA na mazingira ya kifo cha Bilionea maarufu wa Bukoba, Leonard Mtensa aliyefariki saa chache baada ya kufanya mapenzi ndani ya gari kuacha gumzo, gumzo lingine lilitokea wakati wa mazishi yake ambayo yalihudhuriwa na wananchi wengi kutoka ndani na nje ya mkoa, mkanda kamili huu hapa.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mazishi hayo mwanzo mwisho, msiba huo ulikuwa wa pekee kwani haijawahi kutokea kwa yeyote kuzikwa na umati mkubwa kiasi hicho na kusababisha watu wote wasimame kiasi cha kuwafanya askari wa usalama barabarani kufanya kazi ya ziada kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Wananchi wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita. “Msafara ulianzia mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika klabu yake ya Lina’s kisha ukapitia mtaa wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba kisha kuelekea kijiji cha Kyaikailabwa. 
“Ilikuwa si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi kutokea msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani, trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo. 
Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye foleni nyumbani. 
Jeneza likibebwa kuelekea makabulini. 
Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini. 
“Palifunga kabisa, huwezi amini ule msururu wa magari ulianzia Bukoba mjini hadi Kyaikailabwa, magari yenyewe asilimia kubwa yalikuwa ya maana.“Marehemu alikuwa tajiri na baadhi ya marafiki zake pia walikuwa matajiri sasa ilikuwa ni balaa maana magari ya kifahari tupu yalipamba msafara huo. 
Mwili wa marehemu ukiandaliwa kwa ajili ya mazishi. VIGOGO NJE YA NCHI
“Mbali na matajiri na wafanyabiashara wazawa kuhudhuria msiba huo, walikuwepo marafiki wengi wa marehemu kutoka Afrika Mashariki na Kati ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa wakimfahamu marehemu kwa kushirikiana nao kibiashara,” kilisema chanzo chetu. WAKATOLIKI WAKATAA KUMZIKA
Chanzo hicho makini kilidai kuwa, kutokana na mazingira ya kifo na watu waliokwenda kuomba misa ya msiba huo kutokidhi vigezo, viongozi wa kanisa katoliki walikataa kuongoza ibada ya mazishi.
Ilidaiwa kuwa waliokwenda kuomba misa hiyo hawakuwa na sifa za kiimani (hawakuwa wakatoliki) sambamba na kutotumia busara wakati wa kujieleza.
Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu. “Waliokwenda kuomba misa hawakuwa wakatoliki halafu mbaya zaidi hawakuwa na busara wakati wa kujieleza, mapadri wakawagomea kuongoza ibada hiyo,” kilisema chanzo.
Badala yake, inadaiwa kuwa ibada ya kumuombea marehemu iliendeshwa na wakristo wa Kilokole iliyofanyika nyumbani kwake. 
TUJIKUMBUSHE
Marehemu Mtensa aliyeacha mjane na watoto kwa mkewe wa ndoa, alikutwa na umauti Novemba 18, mwaka huu saa chache baada ya kuzidiwa akiwa ndani ya gari lake akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyejulikana kwa jina la Jackline Hassan.
Mwili wa marehemu ukiingizwa kaburini. Kitendawili kingine kilichoteguliwa ni kuhusu msichana Jack, mwenye umri wa miaka 25, ambaye awali iliaminika kuwa ni mpenzi wake aliyekutana naye ghafla tu, lakini inasemekana alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu wa Mtensa na kwamba hata wakati flani alipokuwa akienda Uganda kuwaangalia watoto wake waliokuwa wakisoma huko, alikuwa akiongozana naye. 
Aidha, stori nyingine kutoka huko zinadai kwamba polisi wamekuwa wakitaka kumuachia msichana huyo wakiamini hakuwa na kosa, ingawa hakuna taarifa zozote zilizokwishatolewa hadi sasa kuhusu uchunguzi waliofanya.

No comments: