welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Saturday 22 November 2014

KILICHOMFANYA AUNTY EZEKIEL KUANGUA KILIO MBELE YA WASANII WENZAKE


Msanii wa Filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel hivi karibuni alijikuta akiangua kilio alipokuwa eneo la kuigiza ‘location’ pande za Kijichi jijini Dar baada ya kusumbuliwa na jino ambapo alishindwa kuvumilia maumivu.Diva wa Filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel. Akizungumza  na Amani baada ya kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Aviation, Aunty alisema kuwa  alijikuta uvumilivu unamshinda na kuangua kilio kwani kila alipojaribu kufanya kazi alishindwa.
“Huwezi amini sikupenda hata kuongea na watu, jino naliheshimu sana kwani maumivu yake kama hayajakufika unaweza kuona mtu  anajifanyisha,” alisema Aunty.
Baada ya tukio hilo, Aunty aliyekuwa amejichimbia kwenye kambi ya William Mtitu amesitisha zoezi la kupiga picha hadi hali yake itakapokuwa nzuri.

No comments: