welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Sunday 2 November 2014

CHENI YA SH. MIL. 6 YAMFIKISHA POLISI AUNTY EZEKIEL!

NYOTA wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel ameingia matatani na maafande wa Kituo cha Polisi Pangani, Ilala jijini Dar akidaiwa kutokomea na cheni ya Shabani Limo yenye thamani ya shilingi milioni 6. 
Nyota wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel akiwa Bongo. Kwa mujibu wa chanzo, mwishoni mwa Februari, mwaka huu, Aunty alikwenda kwa Shabani na kuazima cheni hiyo kwa makubaliano ya kuirejesha baada ya muda jambo ambalo hakulifanya na baadaye, Septemba mwaka huu, akasafiri kwenda Marekani kutangaza utalii wa ndani. 
Baada ya kurejea, Oktoba mwaka huu, Shabani alimkomalia Aunty na kufikishana Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar ambapo staa huyo alisema na yeye alimwazima cheni hiyo rafiki yake aitwaye Neema. 
Ilidaiwa kuwa, Neema baada ya kubanwa alikiri na kusema aliiweka bondi cheni hiyo na hapo ndipo danadana zilipoanza hivyo jamaa akaamua kwenda kufungua madai mengine Kituo cha Polisi Pangani. 

Juatano iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari mpaka kituoni hapo ambapo baadhi ya askari walikiri kuwepo kwa kesi hiyo lakini waligoma kutoa namba za kumbukumbu za jalada ‘RB’ wakidai mwenye uwezo huo ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova. SOMA ZAIDI>>>

No comments: