welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Friday 14 November 2014

ANGALIA SABABU INAYOMALIZA VOCHA HARAKA KWENYE SIMU YAKO..


Watumiaji wengi wa huduma ya simu za mkononi wamekuwa wakilalamikia wizi wa pesa unaofanywa na baadhi ya makampuni hayo, leo katika kikao cha Bunge Dodoma Serikali imesema inatambua kuhusu wizi unaofanywa na baadhi ya makampuni ya simu za mkononi na
kutoa tamko namna ambavyo imejipanga kukabiliana na wizi wa aina hiyo.
Akitoa tamko hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amesema Serikali itaanzisha kituo maalum cha kushughulikia malalamiko hayo CCC, kitakachokuwa kinasimamiwa na TCRA.
Akiuliza swali kuhusiana na jinsi Serikali ilivyojipanga kukabiliana na wizi huo Mbunge wa Konde Khatib Said Haji amesema; “… Wizi huu unaofanywa na makampuni ya simu si wizi mkubwa kama ule wa ESCROW.. ni wizi mdogo mdogo unaowaibia Watanzania elfu tano elfu tatu lakini kwa ujumla wake, Mpemba aliyeko Konde akiibiwa elfu tatu, Mnyamwezi wa Tabora elfu mbili, Ukizijumlisha ni mamilioni ya shilingi wanaibiwa Watanzania… Leo watu hao elfu tatu elfu mbili unawaambia wapeleke malalamiko yao, gharama hiyo umeikadiriaje hata mtu huyo akadai malalamiko ya elfu tatu..”

“.. Hivi serikali yenu makini imekuwa wapi muda wote mpaka kukiri kama Watanzania wamekuwa wakiibiwa na bila wenyewe kujijua?, na bado hamna hatua mlizozichukua, ni nani aliyeko nyuma ya pazia hili la kuibia Watanzania na ninyi mkaridhia ama ni yale yaliyosemwa kama CCM ina fund katika wizi huu..?”- Khatib Said Haji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amesema; “…Napenda nikiri tatizo la wizi au dhuluma kwa wateja lipo na ndio lililopelekea tukaweka hizi kanuni ambazo zinaweka adhabu na hatua za kuchukua katika kuchukua katika kudhibiti wizi huo.. Licha ya utaratibu wa kawaida wa kulalamika katika makampuni ya simu, kwa sababu moja ya matakwa ya sheria ni kwamba kampuni za simu zinapaswa kuweka utaratibu wa kuhudumia watekja wake, lakini tumebaini kwamba utaratibu huo una matatizo, unaweza ukapiga simu muda mrefu isipokelewe, unaweza kuambiwa usubiri na wakati unasubiri kulalamika pia unakatwa..
Kwa hiyo Serikali inafahamu hilo, pamoja na hatua tulizozichukua ni kuweka ule mtambo wa kufuatilia mawasiliano ambao moja ya kazi yake sio kufuatilia tu mapato lakini ubora wa mawasiliano.. Kwa kutambua kuwa makampuni ya simu haya wakati mwingine yanachelewa wakati mwigine yanapuuza wateja, kituo hiki ambacho tunakianzisha namba zake zitasambazwa kila mtu atakuwa nayo, kwa hiyo huna haja kusafiri kufuatilia shilingi elfu mbili elfu tatu elfu tano. Kutakuwa na namba ambayo ni bure kupiga..”- January Makamba.
“ Kila utakapopiga kulalamika utapewa namba maalum ya lalamiko lako, na lisiposhughulikiwa hata kitengo cha kampuni ya simu kutoshughulikia lalamiko lako na yenyewe itakuwa sababu ya makampuni hayo kuadhibiwa..”- January Makamba.

No comments: