welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday, 9 October 2014Roberto Di Matteo
Aliyekuwa meneja wa Chelsea na Wesbromwich Albion kwa nyakati tofauti, Roberto Di Matteo sasa amelamba shavu lingine nchini Ujerumani baada ya leo hii klabu ya Schalke 04 kumtangaza kuwa meneja mpya wa klabu hiyo.
Di Matteo, mwenye asili ya nchini Italy, amejiunga na Schalke baada ya aliye kuwa kocha wa timu hiyo, Jens Keller kufungashiwa virago kwa sababu ya matoke mabavu yanayo iandama klbub hiyo tanga ligi kuu nchi Ujermani msimu wa 2014/2015 ianze.
Schalke ipo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Bundesliga wakiwa wamejikusanyia jumla ya pointi nane tu kutoka michezo saba walizocheza ambapo pia wamefanikiwa kushinda mechi mbili pekee kati hizo.


Lakini katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, Schalke ipo katika nafasi ya tatu katika kundi lao baada ya kutoa sare kwenye mechi mbili alizozicheza mpaka sasa ambopo moja kati ya hizo mechi ni ile dhidi ya Chelsea ambayo walitoka sare ya 1-1 dimbani Stanford Bridge.


Kati ya mechi ngumu ambayo Schalke 04 inategemea kucheza ikiwa chini ya Di Matteo ni mchezo ujao wa Novemba 25 dhi ya Chelsea ( klabu bingwa barani Ulaya).

No comments: