welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 29 October 2014

NGALIA PICHA JINSI CHOMBO CHA NASA ROCKET KILIVYOLIPUKA



Roketi ya safari za anga za juu iliyokua ikielekea Kituo cha Kimataifa cha Anga za juu imelipuka wakati ikiruka kutoka jimbo la Virginia nchini Marekani.
Roketi Antares, yenye urefu wa ghorofa 14 ikiwa imetengenezwa na shirika la Orbital Sciences Corp, ililipuka sekunde chache baada ya kuruka katika kituo cha Wallops Flight Facility.
Chanzo cha tatizo la kulipuka kwa roketi hiyo ya mizigo bado hakijafahamika.
Mipango ya kurusha roketi hiyo ya anga za juu Jumatatu, ilicheleweshwa kutoka na boti iliyokuwa karibu na eneo la maji la kurukia roketi hiyo.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwa ya tatu kupewa kandarasi na Shirika la taifa la kusimamia safari za anga za juu la Marekani, NASA.

Roketi hiyo ilitarajiwa kubeba karibu kilo 2,200 za shehena kwa ajili ya wanaanga sita walioko katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
"Tutajua kilichotokea, tunatumaini hivi karibuni, na tutaendelea vizuri na mipango yetu," amesema Frank Culbertson, makamu-rais mtendaji wa shirika la Orbital Sciences.
"Wote tumeona hili jambo likitokea kabla katika shughuli zetu, na wote tumeona kampuni husika zikiimarika kutokana na tukio kama hili, na tutafanya vivyo hivyo."
Roketi kabla ya kuruka

Roketi muda mfupi kabla ya kuruka
Hakuna aliyejeruhiwa, amesema Bwana Culbertson, na kundi la wataalam wachunguzi tayari walikuwa wakipitia data kujaribu kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Amesema, Jumatano asubuhi, kazi ya upimaji wa mabaki katika eneo la tukio ingeanza.
Uchunguzi hautarukia kwenye hitimisho lakini kundi moja la uchunguzi litajielekeza kuchunguza injini za roketi hiyo AJ-26 zilizotumika kuinyanyua roketi hiyo kutoka eneo la kurukia, anasema Jonathan Amos, mwandishi wa BBC wa masuala ya sayansi.
"Kwa kweli hizi ni injini za Kirusi zilizoboreshwa ambazo kwa asili zilitengenezwa kwa ajili ya roketi za Urusi za kwenda mwezini za N-1.

"Zilitengenezwa kufikia viwango vya kisasa, lakini moja ililipuka wakati wa majaribio ardhini mapema mwaka huu."

No comments: