welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday, 8 October 2014

MWAKILISHI WA BONGO MUVI BUNGE LA KATIBA ANUSURIKA KIFO


Mwakilishi wa wasanii katika Bunge Maalum la Katiba (BMK), Paul Mtenda juzikati alinusurika kifo baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na lingine katika eneo la Dumila mkoani Morogoro wakati akirejea jijini Dar es Salaam kutoka Dodoma. 
Mwakilishi wa wasanii katika Bunge Maalum la Katiba (BMK), Paul Mtenda. “Namshukuru Mungu sikuumia kwa sababu nilikuwa nimefunga mkanda, lakini kile kilikuwa ni kifo kwangu,” alisema mwakilishi huyo, mmoja wa wajumbe waliopitisha Katiba Mpya ya nchi inayopendekezwa.Muonekano wa gari hilo baada ya ajali. Kutokana na kunusurika huko, Paul alisema alilazimika kufanya maombi maalum kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kumuepusha na kifo, licha ya gari lake kuharibika vibaya.

No comments: