welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Thursday 9 October 2014

MAKALA YA LEO BILA AJIRA TUTAWEZA?


Ajira imekua gumzo kila sehemu uendapo nchini kwetu hata pia nchi nyingine.wasomi kwa wasiokua wasomi pasenti kubwa wanapitia tatizo hili.tatizo la ajira limevunja myoyo ya wengi na wengine kukata tamaa na kuamua kufanya vitu wasingefanya ili kuweza kujipatia riziki na chakula cha kila siku. Tatizo hili limesababisha mauaji na upotezi wa maisha ya vijana bila hatia na pia kuongeza uhalifu na pia wengine kujiingiza katika mambo tofauti ili kuepuka umaskini. Wanaotafuta kazi ni wengi kuliko wanaotafuta wafanyakazi nah ii umesababisha mashindano makazini na maofisini.
Kinachoshangaza wasio na kazi ni wale ambao wamemaliza masomo yao.tatizo tulilanao kama vijana wa kitanzania ni kua na dharau ya kazi.tunapenda kufanya kujenga jina na sio maisha yetu au kujifunza zaidi na kwasababu ya hili wengi wametupita katika maisha. Hivyo nasimama katika nafasi ya vijana wenzangu kutoa ushauri kwa wenzangu ambao bado mnategemea kazi.chochote chema ambacho unaweza fanya ili kujipatia kipato kifanye na usiangalie watu watasemaje kwasababu hao hao utakapoanza kufanikiwa kifedha watakuja kuchukua mikopo na tusipende kuiga wengine wanachofanya ili nasisi tufanye kama wao.tunaweza tukapambana na tatizo hili kama tutajishusha na kutoa vibuli katika maisha yetu ili tukubali uharisia wa maisha kwasababu ni bora kua na hicho kidogo kuliko kukosa kabisa na kwakusema hivyo sisemi kwamba msiwaze makubwa bali nashauri kwamba tuende kwa hatua katika kila tulifanyalo ili tusijikwae mbele ya safari yetu ya mafanikio.vijana tuna nguvu na tuitumie katika mema yakufuraisha na pia kuendeleza waliotuzunguka na kwa uhai Mungu aliotupa bado matumaini yapo.tumtangulize Mungu mbele katika kila jambo nae atatusaidia katika maisha yetu pia.

Kwa mawasiliano zaidi
0688440029
instagram:ellydavid

No comments: