welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 1 October 2014

HATIMAYE DOKII ATIMIZA AHADI YA ZAWADI YA SHAMBA KWA LUCY KOMBA!


MSANII mkongwe wa filamu Ummy Wenslaus ‘Dokii’ amemkabidhi swahiba wake Lucy Komba, kiwanja chenye ukubwa wa robo hekari, kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni kutekeleza ahadi aliyoitoa kwenye kicheni pati yake.Msanii mkongwe wa filamu Ummy Wenslaus ‘Dokii’. “Mimi naona tunaendana kitabia na Lucy, alinipa kazi moja katika filamu yake ya Yolanda nikiwa kwenye kipindi kigumu sana, hivyo ni rafiki yangu wa kweli maana wengine wanaogopa hata kunishirikisha kwenye kazi zao wanajua nitawafunika,” alisema Dokii.
Msanii mkongwe wa filamu Lucy Komba akiwa na mume wake Stanley.Kwa upande wa Lucy alisema: “Mimi sijawahi kuona urafiki wa namna hii, maana wengine wanatunzana hela kwenye kumbi kitu ambacho siyo sahihi, lakini nashukuru Dokii kanipa kitu ambacho naweza kujivunia maisha yangu yote mpaka wajukuu zangu.”

No comments: