welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 1 October 2014

BIFU LA FLORA, NISHA LAFIKA PABAYA!



WASANII wawili waliowahi kuwa marafiki wa kupika na kupakua, Flora Mvungi na Salma Jabu ‘Nisha’ bifu lao sasa limefika pabaya baada ya hivi karibuni kuwaacha watu midomo wazi kwa kitendo chao cha kupitana kama hawafahamiani.Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’. Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu, Wastara Juma iliyofanyika katika ukumbi wa Dar West uliopo Tabata jijini Dar es Salaam. Wawili hao walikutana mlangoni wakati wa kuingia, lakini Flora alimpita Nisha kama hamfahamu na kama hiyo haitoshi, walipoingia ndani, kila mmoja alikaa meza yake. Wakati sherehe zikiendelea, ukafika wakati wa kufungua shampeni na baada ya tukio hilo, Nisha alipewa jukumu la kuwagawia wageni waalikwa kwa kuwamiminia kwenye grasi zao, lakini alipofika kwenye meza aliyokaa mwenzake, Flora alikataa glasi yake kuwekwa kinywaji hicho.
Msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi. Baada ya tukio hilo, paparazi wetu aliwafuata mastaa hao na kuwauliza kulikoni, na Flora alisema: “Sikumuona Nisha mimi, na shampeni nimekataa kwa sababu huwa siipendi.”
Kwa upande wake, Nisha alisema: “Mimi sikumuona Flora, kuhusu Shampeni mbona nilimimina kwenye glasi zote jamani!”

No comments: