welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Saturday 4 October 2014

BAWACHA WAANDAMANA KUELEKEA IKULU, HALIMA MDEE ASHIKIRIWA NA POLISI JIJINI DAR


 Mwenyekiti  wa BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe kupitia CHADEMA Halima  Mdee akiwa katika maandamano akiwaongoza wanawake wenzake kuelekea Ikulu kumpelekea ujumbe Rais Jakaya Kikwete kwamba hasikubali kuweka saini Rasimu mpya iliyopitishwa juzi mjini Dodoma, maandamano hayo kabla  hayajafika mbali walitawanywa na jeshi la polisi lililotumia maji ya  kuwasha pamoja na kupigwa kwa waandamanaji na kumshika mwenyekiti huyo  Halima Mdee pamoja na wafuasi wake na kupelekwa polisi  Osterbay leo.
 Polisi  wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi leo 
 
Mfuasi wa chadema akishikiliwa na polisi na kupelekwa katika gari la polisi
 

 
Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Osterbay.

 
Halima mdee akizozana  na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari

Wafuasi wa  chadema wakimueleza polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha polisi cha Osterbay wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa mwenyekiti wao Halima Mndee
 
 
Wafuasi wa chadema wakilalamika  kwa polisi
 
Kituo cha polisi cha Osterbay kilikuwa na ulinzi wa kutosha na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia kituoni hapo
 
Polisi wa Osterbay wakizuia gari kupitia 
 
Wakina mama wa chadema wakifika katika eneo la polisi Osterbay
 
 
Viongozi wa chadema wakiomba kuruhusiwa kupita polisi ya Osterbay (Picha na Habari 24)

No comments: