welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Wednesday 8 October 2014

BALIMI EXTRA LAGER YATANGAZA RASMI UDHAMINI WA MASHINDANO YA MBIO ZA MITUMBWI KANDA YA ZIWA KWA MWAKA 2014.

IMG_8275
Dar es Salaam, Jumanne 07 Octoba 2014: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya mbio za mitumbwi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa mwaka huu wa 2014. Mashindano haya ya “kupiga makasia” yanafanyika kwa mwaka wa kumi na tano sasa na yamekuwa na hamasa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa hususani wale ambao ni wavuvi. Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana, kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”. Alisisitiza pia umuhimu wa michezo katika kujenga afya bora.
Edith alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya mitumbwi yatahusisha miji mitano ya kanda ya ziwa kama ratiba inavyoonyesha hapo chini kwa hatua ya awali.
TAREHE MAHALI/MKOA UWANJA
18/10/2014 KIGOMA UFUKWE WA MAGEREZA
01/11/2014 BUKOBA UFUKWE WA SPICE BEACH
08/11/2014 MWANZA UFUKWE WA MWALONI
15/11/2014 KISIWA CHA UKEREWE UFUKWE WA HOTELI YA MONARCH
22/11/2014 MUSOMA UFUKWE WA BWALO LA POLISI
 Washindi watakaopatikana katika miji hii watashindanishwa kwa pamoja ili kumpata mshindi wa kanda. Shindano la kumpata mshindi wa kanda linategemewa kufanyika jijini Mwanza mwanzoni mwa mwezi December. Tarehe 6 Disemba 2014.
Edith Bebwa akizungumzia zawadi za mwaka huu alisema kwamba katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na nne kama zawadi za pesa taslimu kwa washindi. Mpangilio wa zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini;
ZAWADI NGAZI YA MKOA WANAUME NGAZI YA MKOA WANAWAKE NGAZI YA KANDA WANAUME NGAZI YA KANDA WANAWAKE
Mshindi wa Kwanza 900,000 700,000 2,700,000 2,300,000
Mshindi wa Pili 700,000 600,000 2,300,000 1,700,000
Mshindi wa Tatu 500,000 400,000 1,700,000 900,000
Mshindi wa Nne 400,000 300,000 900,000 700,000
Mshindi wa 5 – 10 6 @ 250,000 6 @ 200,000 6 @ 400,000 6 @ 250,000
Edith alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa kanda ya ziwa wajitokeze kwa wingi katika miji iliyotajwa ili kufurahi kwa pamoja katika matamasha haya. Alisisitiza wasisahau mila na tamaduni zao katika kipindi ambacho watu wengi hupenda kuiga tamaduni za kimagharibi. Alimaliza kwa kuwashukuru sana wanywaji wa bia ya Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba waendelee kuitumia kwani ni kupitia mchango wao ndipo pia Balimi Extra Lager inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili yao.

No comments: