welcome

you are welcome dj zombie blog, dodoma tanzania. for latest videos, audios and news.

Tuesday 30 September 2014

Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Geneva

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/0b4ebf51f9366476db61c0c0ebb072cb_XL.jpgAli Akbar Salehi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yuko mjini Geneva, Uswisi kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu na Kongamano la Upokonyaji Silaha. Salehi amebainisha katika hotuba aliyoita jana usiku katika mkutano huo wa Geneva mitazamo ya Iran kuhusu masuala tofauti likiwemo suala la haki za binadamu na upokonyaji silaha. Mkutano huo unafanyika katika hali ambayo, kuwepo vichwa 27 elfu vya silaha za nyuklia ambapo sehemu kubwa ya silaha hizo zinamilikiwa na Marekani na nchi nyinginezo,
kunahesabiwa kuwa tishio kubwa kwa usalama wa dunia. Hata hivyo usalama wa nyuklia haumaanishi kuwa mataifa yazuiwe haki yao ya kisheria ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani. Marekani na nchi kadhaa duniani kwa kutumia uongo na madai yasiyo na msingi zinataka kuyaamulia mataifa mengine mustakbali wao, na kutumia Baraza la Usalama kama wenzo wa kupasisha maazimio ya kisiasa na ya kidhulma ili kudhamini maslahi yao haramu duniani. Kuhusu kadhia ya haki za binadamu pia kuna wasiwasi unaofanana na huo. Hii ni kwa sababu Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zinazodai kuwa ni watetezi wa haki za binadamu, zimegeuza Umoja wa Mataifa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa wenzo wa kisiasa wa kufikia malengo yao ya kikoloni. Hii ni katika hali ambayo fikra za walio wengi duniani zinatambua vyema nafasi ya wazi ya Marekani katika kusambaza silaha za nyuklia, na ulimwengu mzima unajua kwamba Marekani ni nchi pekee duniani iliyowahi kutumia bomu la nyuklia dhidi ya raia wasio na hatia. Pia Israel imetengeneza maghala ya silaha za nyuklia kwa msaada wa serikali ya Washington. Marekani vilevile inashirikiana kwa kiasi kikubwa katika uwanja wa nyuklia na nchi ambazo hazijatia saini Mkataba wa Kuzuia Kuzalisha na Kusambaza Silaha za Atomiki N.P.T. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa sheria za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na Mkataba wa N.P.T, nchi zenye teknolojia ya nyuklia zinapaswa kusaidia mipango ya nyuklia ya amani ya nchi wanachama wa Mkataba wa N.P.T na hazipaswi kushirikiana na nchi ambazo si wanachama. Ukweli ni kuwa, Marekani ambayo kwa mujibu wa baadhi ya ripoti ina karibu vichwa vya nyuklia elfu 10 na ni mkiukaji mkubwa wa mikataba ya kimataifa, inatumia vibaya Baraza la Usalama na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA kama njia ya kuziwekea mashinikizo nchi nyinginezo. Pia inadai kwamba Iran inakusudia kutengeneza bomu la atomiki kwa kutoa madai ya uongo na yasiyo na msingo wowote. Ni wazi kuwa madai ya Marekani na baadhi ya washirika wake wachache yanayotolewa dhidi ya Iran ni sehemu ya malengo ya kisiasa na kipropaganda ya nchi za Magharibi, yenye azma ya kuwapotosha waliwengu kuhusu tishio halisi la amani na usalama linalotokana na kuwepo silaha za nyuklia duniani. Kwa kuzingatia kweli huo inatarajiwa kuwa, Mkutano wa Haki za Binadamu na Kongamano la Upokonyaji Silaha ambao ulianza Jumatatu mjini Geneva na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, itakuwa fursa nzuri ya kubainishwa ukweli huo.

No comments: